Somo LA 2
Somo LA 2 Ili tujue tofauti ya I/ me, He/him She/her We/us They/them; Inabidi kwanza tufaham kitu kinachoitwa kauli. Kuna kauli nyingi ila zinazohusu hapa ni kauli mbili; kauli ya kutenda na kauli ya kutendwa. Labda nifafanue tofauti ya kauli hizi mbili kwa mifano; 1. Juma alikula chakula. (Kauli ya kutenda) 2. Chakula kililiwa na Juma. ( kauli ya kutendwa) - ingawa Juma alitenda kitendo cha 'kula' ktk sentensi zote mbili, huwa hatuangalii ni nani mtendaji ili kutambua kauli mbali huwa tunazingatia kama kile kitu (nafsi) tulichokitanguliza ktk sentensi kimetenda au kimetendwa. - mfano sentensi ya namba 1, nafsi tuliyoitanguliza ktk sentensi ni nafsi Juma , na nafsi hyo imetenda (alikula) hvo sentensi hyo IPO ktk kauli ya kutenda . - sentensi namba 2, tumetanguliza nafsi chakula, na nafsi hyo imetendwa( kililiwa) hivyo sentensi hyo IPO ktk kauli ya kutendwa. - kauli ya kutenda huitwa active voice ilhali kauli ya kutendwa huitwa passive voice. ...
Comments
Post a Comment